🌹 MATENDO YA HURUMA – MWEZI WA ROZARI 🌹
Kaulimbiu: “Tafakari Rozari, Ishuhudie Upendo kwa Matendo.”
Katika mwezi huu mtakatifu wa Rozari, Nguvu ya Rozari inatualika wote kugeuza sala zetu kuwa matendo ya upendo.
Kama Bikira Maria alivyoishi maisha ya kujitoa, nasi tumeitwa kuleta faraja, tumaini na tabasamu kwa wale wanaohitaji zaidi.
🤝 Tenda wema: mtembelee mgonjwa, saidia maskini, fariji waliokata tamaa, toa muda wako kwa upendo.
Kila tendo la huruma ni petali moja katika maua ya Rozari inayompendeza Mungu. 🌺
🙏 “Herufi ya Rozari ni Sala; Maneno yake ni Imani; Lakini Matendo yake ni Upendo.”
Ungana nasi – Nguvu ya Rozari.
Kueneza Upendo, Kuishi Huruma.
#MweziWaRozari #MatendoYaHuruma #NguvuYaRozari #TendaWema #UpendoWaMungu
